Staa wa muziki kutoka Nchini Nigeria Davido, ametunikiwa siku yake ya Novemba 18, huko Mjini Atlanta katika Jimbo la Fulton, Georgia.
Hii ni siku chache tu tangu nguli huyo wa muziki kufanya Tamasha la #AWAY huko Atlanta katika ukumbi wa #StateFarmArena. Kwa mujibu wa Meya wa jiji la Atlanta amesema kuwa Atlanta imetambua umuhimu na mchango wa staa huyo katika kiwanda cha Burudani, hivyo wamemtunuku #DAVIDODAY.