Atalazimika kuhamia Dubai, ili kuacha Sigara

Baada ya mkongwe Snoop Dogg kutangaza kuacha kutumia sigara na Bangi, rapa Meek Mill pia amesema na yeye atafuata nyayo za mkongwe huyo na pia ikiwezekana atahamia Dubai, ilikuwa mbali na matumizi ya Sigara.

Mill amefunguka hayo kupitia mitandao wa X, huku akibainisha kuwa aligundulika kuwa na ugonjwa wa emphysema, hivyo daktari wake akamshauri kuacha kuvuta sigara ili kuepuka kukatisha maisha yake.

“Nitaenda  kuishi Dubai na kuacha kabisa kuvuta sigara… Nitakuwa namfuata ndugu yangu Snoop, Maana daktari wangu amesema nitapata ugonjwa wa emphysema kifuani ikiwa sitaacha kuvuta sigara, kwani nitakuwa napunguza nusu ya maisha yangu,”amendika Mill.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *