ASKARI POLISI WAWILI WAFARIKI KWA KUGONGWA NA GARI KIBAHA

Askari wawili wa Jeshi la Polisi, Izdory George Michael na Rehema Juma Magawa wameaga dunia kwa kugongwa na gari katika barabara kuu ya Dar es salaam – Morogoro, eneo la Maili Moja, Kibaha Mkoani Pwani.

Ajali hiyo ilitokea Agosti 25, 2026 majirq ya saa 1 usiku ikihusisha gari aina ya Toyota Noah lenye namba za usajili T 804 ERM lililokuwa likitokea Dar es salaam kuelekea Mlandizi.

Dereva wa gari hilo, anadaiwa kuwa lilipofika katika kivuko cha Watembea kwa miguu, aliyapita magari mengine yaliyokuwa yamesimama kupisha Watu na kwenda kuwagonga Askari hao.

Izdory Michael alifariki dunia katika eneo la ajali, huku Rehema Magawa akijeruhiwa kichwani na kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Tumbi kwa matibabu na alifariki majira ya asubuhi ya leo Agosti 26, 2026.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *