Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Singida imemhukumu kifungo cha maisha jela askari polisi mwenye Cheo cha Sajenti, David Otiga Sangan baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mwanafunzi mwenye umri wa miaka saba ambaye ni mtoto wake.
Hukumu hiyo imetolewa leo Februari 7, 2024 na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Fadhiri Luvinga baada ya Mahakama kujiridhisha na ushahidi uliotolewa na askari,walimu na daktari aliyefanya vipimo kwa mtoto huyo na kubaini Mwanafunzi Huyo alikuwa akifanyiwa vitendo hivyo.