ASKARI JESHI LA AKIBA WAHIMIZWA LUWA MABALOZI WA AMANI SINGIDA

Na Saulo Stephen – Singida.

Jumla ya Askari 90 wa Jeshi la Akiba, wakiwemo wanaume 62 na wanawake 28, wamehitimu mafunzo ya mgambo yaliyoendeshwa kwa zaidi ya miezi minne katika Kata ya Ulemo, Wilayani Iramba Mkoani Singida.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo, Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida, Suleiman Yusuph Mwenda amewapongeza wahitimu kwa nidhamu na juhudi walizoonyesha hadi siku ya kuhitimisha mafunzo na kuwahimiza kuwa mabalozi wa amani na uzalendo katika jamii wanakotoka.

Aidha DC Mwenda ametumia fursa hiyo pia kuwapongeza Viongozi mbalimbali katika Kijiji cha Kitukutu,kwa ushirikiano na juhudi zao katika kuhakikisha mafanikio ya mafunzo hayo, kwa kushirikiana

Amebainisha kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kutoa kipaumbele kwa vijana waliopitia mafunzo ya mgambo, kuwapa fursa za kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) pamoja na nafasi nyingine za kitaifa na kijamii.

Kwa upande wake, Mshauri wa Mgambo Wilaya ya Iramba, SSGT. Omari Jabu Kidawa amesema kuwa Askari hao wa Jeshi la akiba wamefundishwa masomo mbalimbali yenye lengo la kuwajengea uzalendo, ukakamavu, nidhamu, na utayari kwa majukumu ya kitaifa yanayoweza kujitokeza,” aliongeza mshauri huyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *