Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Aliyesababisha kifo cha Askari apandishwa kizimbani

Mkazi wa Nyasaka Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza, Philipo Mhina (52), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Ilemela mkoani humo na kusomewa shtaka la kuendesha gari kwa uzembe katika barabara ya Umma na kusababisha kifo cha askari wa Usalama Barabarani, WP 3984. Sajenti, Stella Alfonce.

Philipo amesomewa shtaka hilo leo Novemba 10, 2023 katika kesi ya jinai namba 36752/2023 ambapo anadaiwa kutenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 41, 63 (2) (b) na 27 (1) (a) cha Sheria ya Usalama Barabarani sura 168 marejeo ya mwaka 2002.

Akisoma maelezo ya kesi hiyo mbele ya Hakimu mkazi Mwandamizi Amani Sumari, mwendesha mashtaka wa serikali Monika Mweli amesema mshtakiwa alitenda kosa hilo Novemba Mosi, 2023 eneo la Nyamhongoro Wilaya ya Ilemela wakati akiwa anarudisha nyuma gari yenye namba za usajili T.964 BRJ aina ya Mitsubishi Rosa baada ya kukamatwa na kosa la usalama barabarani na alimgonga Sajenti Stella na kusababisha kifo chake.

Baada ya kusomewa shtaka hilo, mshtakiwa amekana shtaka hilo na amerejeshwa rumande kutokana na kutokidhi vigezo vya dhamana ambapo alitakiwa kuwa na wadhamini wawili na barua ya mwenyekiti wa serikali ya mtaa kila mmoja.

Hakimu Sumari, ameahirisha shauri hilo hadi tarehe 23.11.2023 litakapokuja kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali ya shtaka linalomkabili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *