Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Asili ya vazi la khanga

Vazi la khanga huvaliwa maeneo mbali mbali Afrika Mashariki na baadhi ya maeneo ya Afrika ya kati haswa katika maeneo ya pwani kama Dar es Salaam, Mombasa na Zanzibar.

Vazi hili likiwa asili yake ni Zanzibar, lilianzishwa kutokana na ushawishi wa wareno ambapo khanga ya kwanza kuchapishwa ilikuwa khanga yenye rangi nyeusi na nyeupe,mwaka 1860 na jina la khanga hiyo ilijulikana kama khanga Zhamira na baadae vazi hilo likaendelea kukua katika ubunifu mbalimbali.

Licha ya kuibuka kwa nguo nyingine ambazo zinaweza kutumika kama khanga kwa mfano kikoi, mitandio na madira, watumiaji wa Khanga wanadai kuwa bado khanga ina nafasi yake kubwa zaidi ya hizo zote kwa kuwa sasa wabunifu mbalimbali wa nguo wanatengeneza vitu kama; viatu, mikoba na mitindo mbalimbali ya nguo kutokana na khanga, na kila mwanamke ana doti kadhaa za khanga nyumbani kwake na kuna maeneo ambayo.

Katika kisiwa cha Unguja ,Khanga inaelezwa kutumika katika hatua zote za maisha ya binadamu tangu anazaliwa mpaka anakufa.Mtoto anapozaliwa huwa anavalishwa khanga,akiwa katika hatua ya kuingia ujana; wasichana kwa wanaume huvaa khanga na kwenye mazishi khanga ufunika mwili wa marehemu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *