ARUSHA YASHEREHEKEA MIAKA 63 YA UHURU KWA MAOMBI.

Kwenye kusherehekea miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika, Mkoa wa Arusha chini ya Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Paul Makonda umeendesha maombi maalum ya kuiombea Arusha na Tanzania kwa ujumla ikiwa kama sehemu ya maadhimisho hayo ya Uhuru wa Tanganyika.

Maombi hayo yametanguliwa na matembezi ya amani yakiwa na Viongozi wa dini mbalimbali, Viongozi wa Kimila na Viongozi wa Kiserikali wa mkoa wa Arusha nia ikiwa kuuombea mkoa wa Arusha na Tanzania kwa ujumla kuwa na amani na Maisha ya watu yabadilike.

Itakumbukwa Tanganyika ilipata uhuru wake tarehe 9 Disemba 1961, kwenye historia kabla ya uhuru eneo la Tanganyika, Rwanda na Burundi liliunda koloni la Afrika Mashariki ya Kijerumani ambapo baadae ilisimamiwa na Uingereza kuanzia mwaka 1916 mpaka 1961.

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Baba wa Taifa la Tanzania ndiye muasisi wa uhuru huu kupitia chama chake cha Tanganyika African National Union (TANU) kipindi hiko kabla ya kuungana na chama cha  Afro Shirazi Party (ASP) cha Zanzibar na kuzaliwa chama cha mapinduzi Februari 05 1977.

Jambo FM inaungana na Watanzania wote Duniani kukutakia maadhimisho mema ya Uhuru wa Tanganyika wewe Mwanamaisha Fresh.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *