
Hatimaye kampuni ya Apple imezindua simu yao mpya ya iPhone 15, Apple Watch na Airpods kwenye hafla yake ambayo wameiita “Wonderlust” inayofanyika usiku huu leo septemba 12 huko Cupertino, California ambayo inashuhudiwa mubashara na watu zaidi ya milioni 2 Youtube.
Hafla hiyo inafanyika kwenye chuo cha Apple kwenye ukumbi wa michezo wa Steve Jobs. Tukio hilo limekuwa likifanyika kila mwaka kwenye kalenda ya teknolojia, kuanzia mwanzo wa iPhone mnamo 2007.
Apple inaacha rasmi kutumia port na cable ya Lighting ambayo imetumika kwa muda mrefu kwa watumiaji wa iPhone tangia mwaka 2012, hivyo iPhone 15 Pro na Pro Max zitaanza kutumia cable port ya USB type C.
Pia Apple imetambulisha Apple Watch S9 na Apple Watch Ultra 2.