Aliyekua msanii wa Konde Gang, Angela ametangaza kuachana na muziki wa Bongo Fleva na kuamua kugeukia muziki wa Injili kulingana na post zake alizoshare kwenye mtandao wa Instagram leo Desemba 31 2024 muda mfupi kabla ya kuingia mwaka 2025.
Angella alianza kwa kuandika ‘Eh Mungu wangu Asante kwa pumzi ya uhai uliyonipa mpaka siku hii ya leo,pia asante kwa ajili ya wote walioni-support 2024, asante pia kwaajili ya dada zuhura maana amekua baraka kwangu na kwa familia yangu, asante sana kwaajili ya wote waliokuwa pamoja na mimi 2024 Huyu Mungu akawatunze’- Angella
Dakika chache baadae akapost post yenye maneno machache, akiandika ‘Bye bye bongofleva hatutaonana tena Narudi madhabahuni pa Mungu’ – Angella