ANC Chapoteza Viti Vingi,Kuunda Serikali Mseto

Chama tawala cha Afrika Kusini cha African National Congress ANC kimepoteza wingi wa viti bungeni kwa mara ya kwanza mnamo kipindi cha miongo mitatu.

Chama hicho kimehitaji washirika ili kuunda serikali ya mseto, matokeo ya awali ya tume ya uchaguzi yameonyesha chama cha ANC kikipata asilimia 40.2 ya kura huku chama kikuu cha upinzani cha Democtratic Alliance DA kikiwa na asilimia 21.

Wakati chama kilichoanzishwa miezi sita iliyopita na rais wa zamani Jacob Zuma, uMkhonto we Sizwe (MK), kikishika nafasi ya tatu na asimilia 14.5.

Na Chama chenye ushawishi wa Marxist cha Wanaopigania Uhuru wa Kiuchumi (EFF) kimepata asilimia 9.5 ya kurana matokeo rasmi ya uchaguzi huo yatatolewa baadaye leo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *