ANAYETUHUMIWA KUMUUA NA KUMZIKA MUMEWE MIKONONI MWA POLISI


Jeshi la Polisi Mkoani Geita linamshikilia Martha Japhet (44), mkazi wa Kitongoji cha Mzalendo, kilichopo Kijiji cha Mawemeru, Kata ya Nyarugusu, Wilaya ya Geita kwa tuhuma za mauaji ya mume wake Shabani Paschal (55).

Taarifa iliyotolewa hii leo Oktoba 17, 2025 imeeleza kuwa tukio hilo limebainika Oktoba 16, 2025 majira ya saa 7:00 mchana
katika Kitongoji cha Mzalendo, ikidaiwa kuwa Shabani Paschal hakuonekana nyumbani kwake tangu Oktoba 11, 2025.

“Katika mahojiano hayo, mtuhumiwa amekiri kuhusika katika tukio hilo na kueleza kuwa, alimshambulia mume wake kwa kutumia kitu chenye ncha kali sehemu ya kichwani. Baada ya kugundua kuwa amefariki, alichimba shimo ndani ya chumba walichokuwa wanalala, akamzika, akajaza kifusi cha udongo kisha kuweka magunia ya mihogo (udaga) juu yake ili kuficha ushahidi,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Hata hivyo, chunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi umebaini kuwa chanzo cha tukio ni migogoro ya kifamilia na kwamba wanaendela kushugulikia tukio hilo na mara baada ya uchunguzi kukamilika, mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *