Staa wa muziki kutoka Nigeria, Ruger, amesema anapenda kuwa kwenye mahusiano na wanawake wengi kwa wakati mmoja kwa sababu hapendi kuwa peke yake au single, na jambo hilo kwake ni furaha tele.
Ruger alisema, “Kuwa kwenye mahusiano na wanawake zaidi ya watatu, au wanne kwa wakati mmoja ni jambo la kufurahisha, Sipendi kuwa peke yangu, siwezi kusema uwongo. Sipendi kuwa peke yangu au mpweke. “ amesema staa huyo kupitia Afrobeats Podcast ya Adesope Olajide.
Akaongeza ukiachana naye leo jua kuna mwingine anajaza nafasi hiyo.