Kama hujawahi kuona paka wengi wakiwa sehemu moja na kwa wakati mmoja, basi taswira ndio hali iliyopo nyumbani kwa Rachel Kabue, mkazi wa Nairobi Nchini Kenya.
Rachael ambaye ni mama wa watoto watano anabainisha kuwa mwaka 2013 alianza kuwasaidia na kuwaokoa paka walio katika mazingira magumu ambapo alianza na paka mmoja na mpaka sasa anapaka 635.
Akizungumza na TRT, mwanamama huyo ambaye ni maarufu kama “Mama wa Paka Kenya,” amebainisha kuwa kwa sasa paka wamepungua kwani wanakuja kuchukuliwa na baadi ya watu na pia ameanzisha kituo chake cha kulea paka kiitwayo Nairobi Feline Sanctuary, kipo eneo la Utawala, ambalo ni kilomita 20 kutoka jijini Nairobi.
#Chanzo :TRT