Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Amuunguza mikono Mtoto wake kisa kudokoa Chainizi

Maneno thomas (35) mkazi wa Chamagati, wilayani Sengerema, anashikiliwa na Jeshi la Polisi akituhumiwa kumuunguza mikono mwanaye kwa maji ya moto akimtuhumu kudokoa mboga ya majani, aina ya ‘chainizi’.

Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Wilbroad Mtafungwa amesema mtuhumiwa alitenda kosa hilo Julai 30, 2023 baada ya kufika nyumbani na kumuagiza mtoto mwingine apike chakula cha usiku ambapo alijibiwa kuwa mboga imeliwa na mdogo wake Daniel (aliyechomwa).

Ameeleza kuwa mtuhumiwa alichemsha maji na kummwagia katika mikono yote miwili kisha kumfungia chumbani hadi majirani walipoanza kuhoji baada ya kutomuona daniel na walipofuatilia waligundua amefanyiwa ukatili huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *