Amuua mpenzi wake na kumtupa porini

Mwili wa mwanamke mmoja huko nchini Uganda, umekutwa umefariki na kutupwa porini huku ukiwa na majereha kadhaa mwilini.

Mara ya mwisho mrembo aitwaye Rashidah Nakadduh (22) alionekana hai Jumamosi, Septemba 23, alipokuwa sokoni akifanya manunuzi kwaajili ya mpenzi wake ambaye ndiye mtuhumiwa wa mauaji hayo.

Kwa mujibu wa msaidizi wa Msemaji wa Polisi Kampala, Luke Owoyesigyire ameeleza kuwa mwili wa mwanamke huyo umeshambuliwa kwa visu hadi kufa na mwanamume (mpenzi wake), na hata hivyo mwanaume amekimbai baada ya kuutupa mwili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *