Amuua EX-Wake kisa wivu

Jeshi la polisi mkoani Njombe linamshikilia Samwel Nduluhundu (38) mkazi wa Mtaa wa Ramadhani Halmashauri ya mji wa Njombe kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya Felister Danda (24) ambaye alikutwa ameuawa na kutelekezwa katika misitu ya Tanwat huku mtoto wake mwenye umri wa miaka miwili akiwa pembeni yake.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa polisi Mkoa wa Njombe, John Imori akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa mmuaji alidaiwa kutekeleza mauaji hayo kutokana wivu wa kimapenzi baina ya wawili hao.

Kamanda Imori amesema marehemu na mtuhumiwa huyo walikuwa wapenzi lakini baadae marehemu aliamua kukataa kuendelea na mahusiano hayo jambo ambalo mtuhumiwa hakukubaliana nalo.

Kamanda Imori amesema mtuhumiwa alimlaghai marehemu ampeleke kwa mganga wa kienyeji katika Wilaya ya Wanging’ombe atakayetibu tatizo lake la shingo ambalo alikuwa nalo tangu zamani.

“Alhamisi usiku mtuhumiwa alimchukuwa nyumbani kwake marehemu akiwa na mtoto wake kuelekea Wanging’ombe lakini walipofika eneo la msitu wa Tanwat ndipo inadaiwa alitekeleza mauaji hayo,”amesema.

Kamanda Imori amesema polisi walifika eneo la tukio siku ya pili na kukuta mwili wa marehemu, mtoto wake akiwa hai na helmet (kofia ngumu ya pikipiki) ambayo imechukuliwa kwa upelelezi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *