Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Amteka mwanae ili aende soba

Mpenzi wa Alexander ‘AE’ Edwards, Cher ameshtakiwa kwa kuwaajiri wanaume wanne kumteka nyara mtoto wake wa kiume, Elijah Blue Allman katika hoteli waliyokuwa na mke wake mwaka jana.

Nyaraka za mahakama zilizowasilishwa na mke wa Allman zinasema walikaa kwa siku 12 katika hoteli kwa lengo la kusuluhisha ndoa yao, lakini katika siku ya kumbukumbu ya ndoa yao watekaji walikuja na “kumchukua” kwenye chumba cha hoteli hiyo.

“Niliambiwa na mmoja wa wanaume wanne waliomchukua kwamba walikodiwa na mama yake Allman.”

Anasema mpaka sasa hajui hali ya mume wake wala mahali alipo na ana wasiwasi juu yake” kwani amekuwa akipatiwa matibabu katika kituo ambacho hakifahamu.

Allman aliwahi kuzungumza kuhusu matumizi mabaya ya dawa za kulevya na mapambano yake ya uraibu mwaka 2014 na jinsi alivyokuwa akitumia dawa za kulevya tangu akiwa na umri wa miaka 11.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *