Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Ampofua kikongwe kisa kunyimwa mil.5

Mwanamke mmoja aitwaye Laley Renae Maina (26) mkazi wa Texas, amekamatwa na jeshi la polisi baada ya kufanya uharibifu kwenye nyumba ya mzee wa 61, ambaye alimuomba kiasi cha $2,000 sawa na Tsh/=5,010,000.00.

Inaelezwa wawili hao walikutana katika mtandao wa kutafuta wachumba matajiri “Sugar Daddy”.

Mwanaume huyo amewaambia polisi kuwa Madina alifika nyumbani kwake hapo San Antonio bila taarifa majira ya saa 2:30 siku ya Jumanne, lakini alimruhusu aingie ndani, ndipo wakawa wanaongea huku wakipata mvinyo na ghafla alimwomba $2,000. Na yeye akamjibu sina hela hiyo.Kufuatia majibu hayo mrembo huyo alionekana kutofurahishwa nayo hivyo akaanza kufanya vurugu ikiwemo kuvunja vitu vya ndani vya mwanaume huyo.

“Alipomtaka Madina kuacha kuharibu nyumba yake, ndipo mrembo huyo alikuchukua na kumwaga sabuni ya kufulia juu ya kichwa chake, na kumchoma macho na kumpofusha,” kwa mujibu wa polisi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *