Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Ampiga mkewe na kumuingiza panga sehemu za siri

Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara linamshikilia mkazi wa Kijiji cha Makong’onda, wilayani Masasi, Mkoa wa Mtwara, akituhumiwa kumpiga mkewe kisha kumuingizia panga sehemu za siri (njia ya haja kubwa) na kumsababishia majeraha.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 14, 2023; Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Nicodemus Katembo amesema kuwa tukio hilo limetokea Oktoba 8 saa moja jioni katika Kijiji cha Makong’onda.

Baada ya kipigo hicho, inadaiwa mtuhumiwa alichukua panga na kumuingizia sehemu ya haja kubwa na hivyo kusababisha majeraha.

Kwa upande wa Hamis Millanzi ambaye ni Mwenyekiti wa kijiji hicho, amesema: “Nilipewa taarifa na mgambo wa kijiji, nilipofika nilikuta mhanga akiwa anavuja damu miguuni hivyo nilazimika kumuwahisha zahanati ya kijiji ambapo alipewa huduma ya kwanza.”

Mwenyekiti huyo aliendelea kueleza: “Hawa wanandoa wamekuwa wakipigana mpaka wanaumizana kuna wakati huyu mwanaume alichoma moto nyumba wanayoishi, sasa amemjeruhi mkewe, nilishatoa taarifa kwa Mtendaji wa Kata ili tutoe taarifa kwa Jeshi la Polisi.”

kwa upande wake mwanamke aliyefanyiwa ukatili huo amesema “nilipoingia ndani nikamkuta amesimama akanishika shingoni na kuanza kunipiga mpaka nikazimia ambapo kelele za watoto ndio zilileta watu nyumbani na kunisaidia, hataki niende hata chooni ana wivu yaani hata hapa kaniacha peke yangu kwa kuwa yuko Polisi,” amesema mwanamke huyo (jina limehifadhiwa) na kuongeza;

“Kuna wakati ananipiga hadi ananichoma sehemu ya siri, sio mara moja nimekuwa nikimshitaki kwa mwenyekiti, tunasuruhiswa na kusameheana, hii ni ndoa yangu ya tatu, sikutaka kuhangaika ndio maana nilikuwa namsamehe mume wangu, sema ana wivu sana hata shambani nasindikizwa, chooni nasindikizwa.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *