Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Amkata mkewe viganja vya mikoni kwa panga

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara limetoa linaendelea kumtafuta Isuto Mantage mkazi wa kijiji cha Majimoto Wilaya ya Serengeti anayetuhumiwa kwa kosa la kumkata na kuvitoa viganja vyote viwili vya mikono mke wake anayetambulika kwa jina la Kagembe George.



Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Salim R. Morcase imeeleza kwamba tarehe 8/1/ 2024 majira ya saa mbili usiku kulitokea mgogoro baina ya wanandoa hao ambapo walifikia hatua ya kutengana na mtuhumiwa kufungua kesi mahakama ya mwanzo ya kutelekeza familia dhidi ya mke wake tarehe 04/01/2024 akilazimisha waendelee kuishi pamoja na tarehe 08/01/2024 kesi hiyo iliondolewa mahakamani ndipo mtuhumiwa alipomvamia na kumjeruhi mke wake kwa kumkata kwa panga akiwa njiani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *