Mzee mmoja nchini Rwanda anayefahamika kwa jina la Callitxe Nzamwita mwenye umri wa miaka 71 amejitenga kwa kujifungia ndani kwa miaka 55 akidai sababu ni kuogopa wanawake.
Mzee Nzamwita, ameeleza kuwa alikuwa na umri wa miaka 16 tu wakati hofu ya wanawake zilimshinda na hakuweza kuwa karibu nao na aliamua kujenga uzio wa mbao wa futi 15 kuzunguka nyumba yake na bado hajatoka nje ya nyumba yake tangu wakati huo.