Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Amchinja mke wake mjamzito, atoa pacha mmoja na kumpika

Jeshi la Polisi mkoani Tabora linamshikilia Hamis Kulwa (35), mkazi wa Kata ya Uyogo wilayani Urambo kwa tuhuma za kumchinja mke wake mjamzito, kumpasua tumbo kisha kutoa watoto pacha.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Richard Abwao amesema tukio hilo limefanyika Januari 30 mwaka huu saa 11 jioni likihusishwa na imani za kishirikina.

Kamanda Abwa amesema baada ya mtuhumiwa kumpasua mke wake, alitoa watoto pacha kisha kumpika mmoja huku mwingine pamoja na mwanaye mwingine aliyekuwa na miaka miwili, akiwazika.

“Wakati wa mahojiano alidai kuwa aliambiwa kuna watu wametumwa kumchukua mkewe na watoto, wanawapeleka Gambushi [eneo lililoko mkoani Simiyu linaloamika kwa nguvu za giza] kufanya kazi za kichawi usiku na siku si nyingi wangewachukua na kuwaua, ndio maana akaamua awaue yeye mwenyewe,” amesema Kamanda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *