Ally’s yagonga treni, watu kadhaa wahofiwa kufariki

Watu kadhaa wanahofiwa kufariki dunia na wengine kujeruhiwa katika ajali ya barabarani, baada ya basi la kampuni ya Allys Star likitoka Dar es Salaam kwenda Mwanza, kugonga treni katika makutano ya reli na barabara, nje kidogo ya mji wa Manyoni, mkoani Singida.

Ajali hiyo imetokea leo Novemba 29, 2023 majira ya saa 11 alfajiri na kushuhudiwa juhudi za uokoaji zikifanywa na raia pamoja na polisi wa usalama barabarani waliofika eneo la tukio.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *