Afisa wa habari wa klabu ya Yanga, Ally Kamwe rasmi ameruhusiwa kutoka hospitali jana Jumapili Februari 25,2024.
Kamwe alikuwa akipatiwa matibabu kwenye hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam, baada ya kupoteza fahamu siku ya Jumamosi ambapo timu yake ilipata ushindi wa Goli nne dhidi ya CR Belouizdad, ndipo wakati anashangilia ushindi huo kwenye vyumba vya kubadilishia nguo alianguka na kupoteza fahamu.