Lawrence Faucette, mtu wa pili aliye hai kupandikizwa moyo wa nguruwe uliobadilishwa vinasaba kwa ajili ya majaribio, amefariki dunia ikiwa ni wiki sita baada ya kufanyiwa upasuaji.
Chuo Kikuu cha Maryland Medical Center, ambapo utaratibu wa majaribio ulifanyika, kimesema moyo ulianza kuonyesha dalili za kutokufanya kazi katika siku za hivi karibuni.
Mwezi mmoja baada ya upasuaji wake, madaktari wake walisema wanaamini kuwa moyo wake ulifanya kazi vizuri na waliondoa dawa zote ili kusaidia utendaji wa moyo wake.
Katika taarifa iliyotolewa na hospitali hiyo, mke wa Faucette, Ann, alisema mume wake “alijua kwamba wakati wake pamoja nasi ulikuwa mfupi na hii ilikuwa nafasi yake ya mwisho. Hakuwahi kufikiria kwamba angeishi kwa muda mrefu kama alivyoishi.”
Timu ya Maryland mwaka jana ilifanya upandikizaji wa kwanza duniani wa moyo wa nguruwe kwa David Bennett ambaye alifariki miezi miwili baadaye baada ya kupandikizwa.