ALIYEUA MKEWE AKIMTUHUMU KUCHELEWA KURUDI NYUMBANI ADAKWA

Mtu mmoja, Chimaguli Majiyangui Samamba (54), anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga, kwa tuhuma za kumuua mkewe kwa sababu ya kuchelewa kurudi nyumbani.


Taarifa ya Kamanda wa polisi Mkoni humo imeeleza kuwa, Chimaguli ambaye ni Mkulima na Mkazi wa Ugede Songambele anadaiwa kutenda kosa hilo Oktoba 8, 2025 majira ya saa 12:00 jioni katika Kitongoji cha Ugede, kilichopo kata ya Salawe, Tarafa ya Nindo Wilaya na Mkoa wa Shinyanga.

Moshi Paulo John (47), ambaye naye ni Mkulima na Mkazi wa Ugede-Songambele aligundulika kuuawa na mwili wake kufukiwa kwenye shimo lililopo jirani na nyumbani kwake.

Oktoba 1, 2025 majira ya saa 4:00 usiku marehemu Moshi Paulo John akiwa

nyumbani kwake aligombana na mume wake aitwaye Chimaguli Majiyangui Samamba, (54), Mkulima na Mkazi wa Ugede_Songambele ugomvi uliotokana na kuchelewa kurudi nyumbani kwa marehemu kwani usiku huo alirudi nyumbani toka matembezini na kumkuta mumewe
nyumbani,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *