ALIYETANGAZA KUUZA MTOTO AIBUKA, ASEMA ILIKUA ‘CONTENT’ TU.

Kwa zaidi ya saa 20 zilizopita Kijana anaejulikana kama jideboy_tz kupitia mtandao wa Tiktok alijirekodi video nyingine na kuipost akisema kuwa nia yake haikuwa kumuuza Mtoto huyo bali alikua akitengeneza tu maudhui ya mtandaoni.

Kwenye video yake ameonekana akisema “Jamani Watanzania nimekuja mbele yenu, huyu ni Mtoto wa Dada yangu naona wengi mmecomment sana, mimi huyu Mtoto ni damu yangu, nilichokuwa nakifanya jana ilikua ni ‘content’ kwahiyo mnaonihisi vibaya mimi siko huko, naomba mnisamehe kwa wale niliowakwaza”

Hata hivyo tayari Msemaji wa jeshi la Polisi Tanzania, David Misime amesema Jeshi hilo limetangaza kumsaka popote alipo kijana huyo ili wamuhoji.

Unaweza kuitazama video hiyo kwa kubonyeza hapa chini..

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *