Khamis Luwoga (45) aliyekuwa akikabiliwa na shitaka la kumuua mke wake, Naomi Marijani na kisha kuuchoma mwili wake kwa kutumia magunia mawili ya mkaa. amehukumiwa kunyongwa.
Hukumu hiyo, imesomwa hii leo Februari 26, 2025 na Jaji Hamidu Mwanga Wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa.

Ushahidi huo ulitolewa na mashahidi 14 wa upande wa Jamhuri, ambao waliweza kuthibitisha pasipo shaka kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo.