Timu ya Young Africans (YANGA) yenye maskani yake mitaa ya jangwani Jijini Dar es salaam, Leo Disemba 11 2024 imemtambulisha aliyekuwa mchezaji wa Simba kwa nafasi ya beki wa pembeni Israel Patrick Mwenda kama mchezajiwao mpya klabuni hapo akitokea Singida Black Stars yenye maskani yake Mkoani Singida.
Israel Mwenda ambaye anachezea nafasi ya beki wa kulia na anayeweza kucheza nafasi ya beki wa kushoto anatarajiwa kuja kusaidia nafasi ya beki wa kulia na kushoto, Wachambuzi wa Michezo wanasema pia anakuja kuwapa changamotoKouassi Attohoula Yao, Shadrack Boka, Nickson Kibabage na Kibwana Shomari ambao wameonekana kuandamwa na majeraha ya mara kwa mara.