Aliyejinyonga akidhani amemuua mkewe sababu yatajwa

Jeshi la polisi Mkoa wa Geita limethibitisha kutokea kwa tukio la Mwanamke Mmoja aliyefahamika kwa jina la Justina Poul (34) mkazi wa mtaa wa 14 Kambarage Kata ya Buhalahla Halmashauri ya Mji wa Geita aliyenusurika kuuwawa na mme wake Martine John (40) baada ya kumjeruhi shingoni na mikononi kwa kumkata na Panga kisha na yeye kujinyonga.

Kaimu Kamanda wa polisi Mkoa wa Geita ACP Adam Maro amesema mwanaume huyo alikutwa kwenye chumba walichokuwa wamepanga akiwa amejinyonga huku mkewe akiwa amejeruhiwa kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo shingoni, mikononi pamoja na begani .

Kamanda huyo amesema kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa mapenzi uliopelekea ugomvi wa kifamilia kati ya wanandoa hao na kupelekea mwanaume huyo kuchukua maamuzi ya kutaka kumuua mkewe baada ya kumjeruhi na kupoteza fahamu huku damu zikiwa zimetapakaa chumbani akazani ameua na yeye kuamua kujinyonga,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *