Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Aliyehukumiwa miaka 22 jela kwa kukutwa na vipande vya nyama ya swala aachiwa huru

Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Iringa imemuachia huru, Maria Ngoda ambaye awali alihukumiwa kifungo cha miaka 22 jela kwa kukutwa na vipande 12 vya nyama ya swala.

Uamuzi huo umetolewa leo Februari 16, 2024 na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Elvin Mgeta ambaye amesema kuwa kutokana na hoja zilizowasilishwa na mkata rufani, Maria hana hatia na yupo huru.

Maria alihukumiwa kifungo cha miaka 22, Novemba 3, 2023 na Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa, Said Mkasiwa baada ya kumtia hatiani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *