Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema Jeshi la Polisi linamshikilia kijana mmoja anayedaiwa kuchoma duka la Nely Mabegi lililopo Mwenge jijini Dar es Salaam na kupelekea moto kusambaa kwenda maduka mengine na kusababisha hasara kubwa kwa wafanyabishara wa maduka 32 katika eneo hilo na kueleza Kuwa atafikishwa mahakamani.
Chalamila amebainisha hilo leo Disemba 8,2023 baada ya kutembelea eneo la maduka hayo yaliyoungua juzi , huku akiwataka wafanyabishara hao kuwa watulivu wakati Serikali inalifanyia kazi suala hilo.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa maelekezo yake ambapo Ofisi yake ya Wilaya ya Kinondoni imemhakikishia kupokea maagizo na kuyatekeleza kwa mslahi mapana ya Umma.