Aliyechinja mama na mtoto akamatwa

Baada ya msako mkali hatimaye Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro limefanikiwa kumkamata Selemani Sita (25) ambaye anadaiwa kumchinja Mama na Mwanae Wakazi wa kijiji cha Mavimba Kata ya Milola Wilayani Ulanga Mkoani Morogoro kwa kutenganisha vichwa na viwiliwili kisha kuondoka na vichwa hivyo na kwenda kuvitupa Mtoni.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro, Alex Mkama amesema Selemani alifika katika nyumba hiyo kwa lengo la kutafuta kazi ya kulima na aliishi kwa muda wa wiki mbili kisha kutekeleza tukio hilo, ambapo amesema baada ya kumkamata Selemani aliongozana na Polisi hadi alikotupa vichwa hivyo katika Mto Ulali uliopo katika Kijiji hicho ambapo kwa sasa upelelezi unaendelea na utakapokamilika atafikishwa Mahakamani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *