Aliyecheza kimahaba na Omah Lay ajitetea

Wiki iliyopita story kubwa ni juu ya mrembo kutoka Nigeria, kupanda jukwaani na staa wa muziki Omah Lay na kuanza kucheza hali ambayo ilizua taharuki na ikapeleka mpenzi wake aliyeenda naye kwenye shoo hiyo kuamua kuondoa ukumbini hapo.

Sasa mrembo huyo katika video aliyoachia mtandaoni ameomba radhi kwa mpenzi wake na kuelezea kuwa yeye ndiye aliyelipia shoo hiyo kwenda na mpenzi wake lakini staa huyo ni msanii wake pendwa.

“Mpenzi wangu hakununua tiketi mimi ndiye niliyemnunulia Tiketi mimi na mtu wangu kwenda kwenye Tamasha la Omah Lay, Omah Lay ni msanii ninayempenda na nilifurahi sana na kucheza naye,”amesema mrembo huyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *