ALIYECHAPISHA MTANDAONI VITISHO KWA PADRI KITIMA AKAMATWA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaama, limemkamata kwa mahojiani Frey Edward Cossey (51), ambaye alichapisha andiko la vitisho kwenye mtandao dhidi ya Padre Charles Kitima siku chache kabla ya tukio.

Leo Mei 5, 2025, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Saalam, Jumanne Muliro kupitia taarifa yake ameeleza kuwa pia upelelezi wa shauri la Padri Kitima bado unaendelea huku watu wawili wakidaiwa kuhusika na tukio hilo.

Aprili 30, 2025 majira ya usiku Padri Kitima alishambuliwa akiwa Kurasini katika Makao Makuu ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), na hadi sasa bado anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Agakhan jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *