ALI KAMWE WA YANGA AFUNGUKA BAADA YA YANGA KUTOA DROO NA TP MAZEMBE YA KONGO.

Mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa klabu bingwa Afrika kati ya TP Mazembe ya Kongo na Yanga ya Tanzania, mchezo uliotamatika kwa suluhu ya goli 1-1,  Msemaji wa Klabu ya Yanga Ali Kamwe kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika ‘kIt’s True … Tumepata Pointi 1️ muhimu sana Leo kwenye Kundi Letu. Pointi 1 iliyobeba matumaini Makubwa sana kwenye safari yetu CHAMPIONS LEAGUE Msimu huu’ – Kamwe.


‘Presha kubwa kwenye vifua vya wachezaji na Benchi la Ufundi imeshuka Leo.. Naamini kabisa hii mechi ya Leo ndio TURNING POINT yetu Msimu huu, Sasa Turudi kwenye LIGI KUU kwa nguvu kubwa Wananchi’ . – Kamwe

‘Tuna mchezo mgumu mbele dhidi ya Mashujaa utakaopigwa Alhamis ya Tarehe 19 pale KMC COMPLEX,Huu ni mchezo mgumu na muhimu kwa sababu umebeba POINTI 3️⃣ muhimu kwetu katika safari Yetu ya kurudi Kileleni mwa Msimamo wa Ligi’ – Kamwe

‘Tusimamame pamoja Wananchi. Tuanze maandalizi ya nguvu kwenye Matawi yetu na kuhakikisha Tunakuja kwa wingi KMC kuwapa nguvu wapambanaji wetu, Kazi ndio kwanza imeanza! Hakuna kuchoka👊🏼’ – Kamwe

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *