Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi imewapeleka kwenye Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Ofisa Habari wa klabu ya Yanga, Ali Kamwe na Ofisa Habari wa klabu ya Kagera Sugar, Hamis Mazanzala
Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi Kuu imesema maafisa hao wamedaiwa kutenda kosa hilo kupitia machapisho ya kwenye kurasa zao za mtandao wa kijamii.

Aidha, Bodi pia imewakumbusha Maofisa Habari na Wasemaji wa Vilabu vyote Nchini kuzingatia kanuni za ligi na za maadili wakati wote wanapotekeleza majukumu yao.


