Ali Kamwe azimia Uwanjani.

Afisa habari wa Klabu ya Yanga, Ali Kamwe anadaiwa kuanguka na kupoteza fahamu baada ya mchezo huo kumalizika huku timu yake ikiwa na ushindi wa Goli nne dhidi ya CR Belouizdad.

Kamwe amekumbana na hali hiyo leo Februari 24, 2024 wakati akishangilia ushindi huo kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ambapo ameanguka na kupoteza fahamu.

Kamwe amechukuliwa na kutolewa nje vyumba hivyo kisha kupelekwa hospitali huku akiendelea kupatiwa matibabu akiwa ndani ya gari la wagonjwa.

Katibu wa Madaktari wa Tiba za Wanamichezo nchini, Dr Juma Sufian amethibitisha tukio hilo huku akiomba apewe muda kwani yupo kwenye harakati za kumsaidia msemaji huyo.

#Chanzo:#mwananchi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *