Kunako tetesi za usajili, inaelezwa kupitia mitandao wa Daily Mail kuwa klabu ya soka ya Al-Nassr, wanajipanga kwa dau la kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Brazil Casemiro, 31, na beki wa zamani wa England Aaron Wan-Bissaka,huku Manchester United ikijiandaa kuwauza baadhi ya nyota wake wanaolipwa pesa nyingi.
Pia Al-Nassr tayari wamekataa ofa ya pauni milioni 20 kumnunua beki wa kulia wa Tottenham na Brazil Emerson Royal, 25, na wanamtazama Wan-Bissaka kama mbadala wake.