Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Akiua asinyongwe, afungwe miaka 90

Baadhi ya wakazi mkoani Lindi, wamependekeza maboresho ya sheria za haki jinai nchini ikiwamo mtu anapofanya kosa la mauaji asihukumiwe kunyongwa bali apewe adhabu kubwa kama kifungo cha miaka 70 hadi 90 gerezani.

Wametoa maoni yao mbele ya wajumbe wa Tume ya Haki Jinai, na kuongeza kuwa kumekuwa na uonevu unaofanyika katika mnyororo huo ambao utamalizwa kwa marekebisho ya sheria na muundo.

Wakazi hao wamesema mfungwa anayekaa gerezani mpaka anazeeka na kushindwa kutembea iangaliwe namna ya kumruhusu arudi uraiani kwa sababu unakuwa mzigo kwa wenzake.

Aidha wamelalamikia kitendo cha mahakama kuwataka watu kufikisha malalamiko yao kwa kutumia lugha ya Kiingereza wakidai wengi hawajasoma na hawajui lugha hiyo vizuri na kwamba suala hilo linanyima haki.

One response to “Akiua asinyongwe, afungwe miaka 90”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *