Denis Kazungu ambaye ni raia wa Rwanda, amekiri kosa mahakamani la kuwaua watu 14 na kuwazika jikoni.
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa Kazungu mwenye umri wa miaka 34 aliwaua watu hao ambao ni Wanawake 12 wanaofanya kazi ya kuuza miili yao pamoja na Wanaume wengine wawili na kuwazika katika shimo alilochimba jikoni kwake kwenye nyumba aliyokuwa amepanga.
Polisi nchini Rwanda waligundua uhalifu huo baada ya Kazungu kufukuzwa kutoka kwenye nyumba hiyo kutokana na kushindwa kulipa kodi kwa muda wa miezi saba.
Katika taarifa yake ofisi ya upelelezi ya Rwanda imesema Kazungu aliwarubuni watu hao ambao walikuwa wakifanya biashara wa ngono ili waende nyumbani kwake na walipokwenda ndipo alipofanya mauaji hayo.
Katika utetezi wake Kazungu alidai kuwa alifanya mauaji hayo baada ya kubaini watu hao walimuambukiza Virusi vya Ukimwi kwa makusudi, utetezi ambao hata hivyo haukutoa uthibitisho.