Staa wa filamu kutoka nchini Nigeria, Chinedu Ikedieze maarufu kama Aki amefunguka kuwa watu wanamchukulia poa na kujua hana elimu kwa sababu ya nafasi anazoigiza.
Aki amefunguka hayo kupitia mahojiano aliyofanya na Chude Jideownwo kupitia With Chude, “Kutokana sehemu ninazocheza kwenye filamu, baadhi ya watu wanadhani sijasoma, mama aliniambia niende shule nisome kwa bidii ili nifanikiwe kwa sababu siwezi kuwa fundi seremala au fundi matofali kwa sababu ya udumavu wangu/.ukuaji.”
Muigizaji huyo, ana Stashahada ya Juu ya Kitaifa (HND) katika sanaa ya uigizaji, na pia shahada ya Mawasiliano ya Umma kutoka Taasisi ya Usimamizi na Teknolojia.