Mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Hamis Lidonge (31) mkazi wa Kitongoji cha Ukombozi, Kata ya Mahurunga katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara amefariki baada ya kunywa sumu chanzo kikidaiwa ni kuachwa na mpenzi wake.
Kamanda wa Polisi mkoani Mtwara, Nicodemus Katembo amesema tukio hilo limetokea Februari 16, 2024 na uchunguzi uliofanywa umebaini kifo chake kimesababishwa na sumu, lakini bado haijabainika aina ya sumu hiyo.
Akisimulia tukio hilo, baba mdogo wa marehemu, Said Athuman amesema ndugu yake alikuwa akiishi nyumba moja na mpenzi wake na siku tatu kabla ya tukio hilo alirudi nyumbani akidai kufukuzwa na mpenzi wake na ndipo baadaye alipochukua uamuzi huo.