Ajinyonga hadi kufa baada ya baba yake kukataa kupokea mahari

Binti mmoja aliyefahamika kwa jina la Loli Manjale mwenye umri wa miaka 17 mkazi wa mtaa wa Kidinda kata ya Bariadi Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kipande cha kanga kwenye mti uliyokaribu na nyumba ambayo haijakamilika kujengwa.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wameeleza sababu iliyopelekea binti huyo kujinyonga kuwa ni kutokana na baba yake mzazi kukataa kupokea mahari iliyotolewa na kijana aliyetaka kumuoa.

Lucas Gulai ni mwenyekiti wa mtaa wa Kidinda amewasihi wazazi kuwasikiliza watoto wao na kutowalazimisha kuolewa na watu wasiowataka na badala yake wawaruhusu kuolewa na watu waliowachagua wenyewe.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Simiyu ACP. Maulid Shaba amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa Jeshi la Polisi bado linafanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha tukio hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *