Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Ajeruhiwa kwa kukatwa mapanga na mtu asiyejulikana

Mwanamke mmoja aitwaye Ngw’anza John mwenye umri wa miaka 50 mkazi wa kijiji cha Kilugala kilichopo kata ya Nhobora wilayani Itilima Mkoani Simiyu amejeruhiwa kwa kukatwa mapanga na mtu asiyejulikana maeneo ya kichwani na kwenye vidole vya mikono na kusababisha vidole viwili kukatika.

Tukio hilo limetokea nyumbani kwa mwanamke huyo ambaye alikuwa na mtoto wake mdogo ambapo hakuweza kumtambua mwanaume aliyemkata na panga.

Mwenyekiti wa kijiji cha Kilugala Maduhu Kome ameiasa jamii kutokaribisha wageni ambao hawajawatolea taarifa zao katika uongozi wa kijiji huku akiiomba serikali kuimarisha ulinzi katika kijiji hicho sambamba na kumuhamisha mama huyo mara baada ya kutoka hospitalini.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Nhobora Mbuke Ndaki ameeleza kusikitishwa kwake na tukio hilo huku akiiombaserikali kumsaidia mama huyo ili awe salama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *