Watu watatu wamefariki dunia katika ajali iiliyohusisha magari mawili baada ya kugongana uso kwa uso katika Kijiji cha Mbala, Kata ya Vigwaza Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Ajali hiyo lmetokea saa tatu usiku wa kuamkia Oktoba 24,2023 ambapo gari dogo aina ya Kluger yenye namba za usajili T.478 DCQ ikitokea Iringa kwenda Dar es Salam likiwa na watu 7 wa familia moja iligongana na gari lenye namba T.851 AQC aina ya Scania iliyokuwa ikitokea Dar es Salam kwenda Morogoro.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Pius Lutumo amesema katika ajali hiyo watu wanne wamejeruhiwa na wanaume wengine wawili ambao hawajafahamika majina yao.
Kamanda Lutumo amesema majeruhi na waliofariki wote walitoka kwenye gari ndogo iliyokuwa ikitokea Iringa kwenda Dar es Salam ambayo ilikuwa imepakia ndugu wa familia moja.
Ameeleza kwamba chanzo cha ajali hiyo ni gari ndogo kutaka kuiyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari na hivyo kugongana uso kwa uso na Lori hilo ambalo lilijaribu kukwepa gari ndogo bila mafanikio.