Ajali yaua familia moja

Watu watatu wa familia mnoja wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa kwenye ajali ya gari iliyohusisha gari aina ya Toyota Alphard na Lori iliyokuwa ikitokea katika Kijiji cha Mbwewe wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Pius Lutumo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo leo Desemba 28, 2023 majira ya saa 12 alfajiri, ambapo amesema yupo njiani kuelekea katika eneo la tukio na kwamba atalizungumzia baadaye.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Albert Msando kupitia mitandao wa kijamii amesema kuwa waliofariki ni familia ya Diwani wa Kata ya Kabuku, Halmashauri ya Wilaya Handeni mkoani Tanga, Nurudin Semnangwa ambapo amepoteza mke, mtoto na dada wa kazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *