Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Dodoma, Mrakibu Rehema Jeremia Menda amesema hawakubaini mara moja chanzo cha moto uliozuka katikati mwa jiji la Dodoma hii leo Januari 21, 2025.
Menda amesema moto huo uliozuka majira ya saa moja asubihi na ambao walifanikiwa kuuzima, ulikuwa ukiwaka kwenye Maduka 14 yaliyopo barabara ya nane na kuzua taharuki.
Amesema, “tulipokea taarifa kwamba kuna moto na tulikuta moto upo hatua ya tatu kuelekea ya nne, hatuwezi kubaini tatizo maana tulikuta moto umeenea nyumba nzima, wapiganaji waliendelea na jitihada za kuuzima na tuliudhibiti.”
Aidha, Kaimu Kamanda Menda ameongeza kuwa majengo yaliyoungua ni yale ambayo yalijengwa kabla ya uhuru na ni chakavu na kwamba tukio hilo limeleta athari kwa baadhi ya maduka licha ya kwamba waliokoa baadhi ya vitu na kuhakikisha moto hauendi katika nyumba zingine.