Jambo La Leo

Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Ajali ya basi yauwa wawili na kujeruhi 50

Watu wawili wamefariki na wengine 50 kujeruhiwa baada ya basi dogo aina ya Tata lililokuwa linatoka Kigogo Fresh, Pugu Jijini Dar es salaam kuelekea Mloka Wilayani Rufiji Mkoani Pwani kupitia Kisarawe, kupinduka nje kidogo ya Kisarawe Mjini na kuingia Mtoni usiku wa kuamkia leo Desemba 19,2023.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya kisarawe Dkt. Risasi Rajabu amesema baadhi ya majeruhi waliopata majeraha madogo wameshawaruhusu na wengine wanaendelea kuwapatia huduma na majeruhi 7 wamewapatia rufaa ya kwenda Hospitali ya Rufaa Muhimbili.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na amefika Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe usiku wa kuamkia leo kuwapa pole na kuwajulia hali majeruhi hao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *